Idadi ya vifo kutokana na COVID-19 Kenya yapita 1,000 huku watu 685 wapya wakiugua

- Mombasa, Nairobi na Nakuru ndio gatuzi zilizorekodi visa vingi: 203, 202, na 95 mtawalia - Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema visa hivyo vipya vimeongeza idadi jumla ya maambukizi nchini kuwa 55,877

- Mombasa, Nairobi na Nakuru ndio gatuzi zilizorekodi visa vingi: 203, 202, na 95 mtawalia

- Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema visa hivyo vipya vimeongeza idadi jumla ya maambukizi nchini kuwa 55,877

- Miongoni mwa wale ambao wamethibitishwa hii majuzi kuwa na COVID-19 ni ikiwemo Spika wa Bunge la Kaunti ya Machakos Florence Muoti Mwangangi

- Rais Uhuru Kenyatta anatazamiwa kuandaa mkutano wa dharura Novemba 4, kujadili kuhusu kuongezeka kwa maambukizi na vifo kutokana na ugonjwa huo

Habari Nyingine: Mamake katibu Mercy Mwangangi aambukizwa coronavirus

Wizara ya Afya siku ya Jumapili, Novemba 1, iliripoti kuwa watu 685 wapya wamepatwa na virusi hatari vya corona kutoka kwa sampuli 4,433 zilizopimwa ndani ya saa 24.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema visa hivyo vipya vimeongezea idadi jumla ya maambukizi nchini kuwa 55,877.

Kufikia sasa, tangu kisa cha kwa kwanza kuripotiwa nchini, yamkini sampuli 699,520 zimekaguliwa.

Habari Nyingine: Jamaa akamatwa kwa 'kusumbua' maiti makafani

Kutoka kwa visa hivyo vipya, 659 ni Wakenya nao 26 ni raia wa kigeni ambapo 449 ni wanaume na 239 wanawake.

Mgonjwa mchanga zaidi ni mtoto wa miaka miwili na mzee zaidi akiwa na miaka 81.

Kagwe pia alitangaza kuwa wagonjwa wengine 231 wamepona ugonjwa huo, 130 kutoka kwa mpango wa matibabu ya nyumbani wengine 101 walikuwa wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini

Idadi jumla ya waliopata nafuu sasa ni 37,194 lakini kwa bahati mbaya wagonjwa 17 wameangamizwa na janga hilo na kuongezea idadi ya vifo kuwa 1,013.

"Rambi rambi zetu kwa familia na marafiki za wale ambao wamepoteza maisha yao,"alisema Kagwe.

Habari Nyingine: Kura imeisha chapeni kazi, Rais Magufuli aambia Watanzania

Waziri huyo alifichua kwamba kuna wagonjwa 1,271 ambao wamelazwa katika hospitali tofauti nchini huku 4,806 wakipokea matibabu nyumbani.

Wagonjwa 53 wamelazwa katika chumba cha wagongwa mahututi (ICU), 31 kati yao wamo katika hali mbaya 22 kati yao wamewekwa kwenye mashine ya oksijeni.

Wagonjwa 46 wametengwa katika chumba tofauti na wanaongezewa oksijeni lakini hali yao sio mbaya huku 17 wakiwekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi zaidi(HDU).

Visa vya maambukizi katika kaunti

Mombasa, Nairobi na Nakuru ndio gatuzi zilizorekodi visa vingi: 203, 202, na 95 mtawalia, Busia 95, Nakuru (18), Kiambu (18), Bungoma (18), Kilifi, Kisumu na Embu visa 17 kila mmoja, Kajiado (15), na Kakamega 14.

Visa vingine viliripotiwa Kwale (8), Machakos (6), Kirinyaga (5), Kericho (4), Murang’a (4), Taita Taveta, Turkana, Nyandarua na Tana River visa vinne kila mmoja, Homabay (3), lsiolo (2), Kisii (2) na Garissa (kisa kimoja).

Katika taarifa tofauti, TUKO.co.ke iliripotia kuwa Miongoni mwa wale ambao wamethibitishwa hii majuzi kuwa na COVID-19 ni ikiwemo Spika wa Bunge la Kaunti ya Machakos Florence Muoti Mwangangi .

Spika huyo ambaye ni mama yake mzazi Katibu Mkuu Mwandamizi wa Afya Mercy Mwangangi kwa sasa yuko karantini

Rais Uhuru Kenyatta anatazamiwa kuandaa mkutano wa dharura Alhamisi, Novemba 4, kujadili kuhusu kuongezeka kwa maambukizi na vifo kutokana na ugonjwa huo.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjbYV0hJRmoJ2ZlJ56uq2Mr6Cfp12gwrW7ypqlmmWelnqku9Wim2ZpaWK4prrYmmSymaCewaJ5kGlnaWWYqri2edaaq65lZm2CbsPAqbCaZaeWuKrBxq6YZ6Ckork%3D

 Share!