Wenyeji wa magari katika jiji la Nairobi na mazingira yake watahitajika kugharamika zaidi hasa kuhusiana na uegeshaji magari.
Serikali ya kaunti ya Nairobi imeongeza ada ya kuegesha magari kutoka KSh 200 hadi KSh 400 baada ya mswada huo kupitishwa katika bunge la kaunti Septemba 15.
Mkurugenzi mkuu wa uegeshaji magari jijini Tom Tinega alisema ada ya uegeshaji magari itagawanyika katika sehemu tatu.
Habari Nyingine: Chuo Kikuu cha Maseno chafungwa kwa muda kufuatia mgomo wa wanafunzi
Habari Nyingine: Inspekta Mkuu azirai na kufariki dakika chache baada ya kutua JKIA kutoka Japan
Sehemu ya kwanza itakuwa katikati mwa jiji ambapo wenyeji magari watahitajika kulipa ada ya KSh 400.
Wale watakao kuwa katika sehemu ya pili ni wale wa mitaa ya Westland, Upper Hill, Community, Ngara, Highbridge, Gigiri, Kilimani Mwiki na South B na watakuwa wakilipa ada ya KSh 200.
Wenyeji magari katika sehemu ya tatu watahitajika kulipa KSh 100, maeneo ambayo hayako karibu na jiji.
Mabasi ambayo hayatumiki kwa uchukuzi wa umma yatahitajika kulipa ada ya KSh 1000 katika uegeshaji magari.
Read: ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690
Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjZ4R3hZBmmJ2ZXa6ubrfUnp6eq5iWeq6txpqpomWanrequshmpZqhoqSvqnnYmqann5WvxKJ6x62kpQ%3D%3D