Ajali barabarani Kericho: Watoto 9, wanawake 15 na wanaume 31 wafariki

- Idadi ya watu waliofariki kwenye ajali mbaya ya barabarani eneo la Fort Ternan, Kericho imeongezeka hadi 55 - Manusura wawili walifariki baadaye walipokuwa wakipokea matibabu hospitalini - Basi lililohusika kwenye ajali hiyo, linasemekana lilikuwa limebeba abiria wengi kupita kiasi wakati ajali hiyo ilipofanyika

- Idadi ya watu waliofariki kwenye ajali mbaya ya barabarani eneo la Fort Ternan, Kericho imeongezeka hadi 55

- Manusura wawili walifariki baadaye walipokuwa wakipokea matibabu hospitalini

- Basi lililohusika kwenye ajali hiyo, linasemekana lilikuwa limebeba abiria wengi kupita kiasi wakati ajali hiyo ilipofanyika

- TUKO.co.ke inafahamu kuwa basi hilo lilikuwa likiendeshwa kwa kasi na lilikosa mwelekeo lilipofika kwenye mteremko mkali

Idadi ya watu waliofariki kwenye ajali mbaya ya barabarani eneo la Fort Ternan katika barabara kuu ya Kisumu kuelekea Muhoroni sasa imefikia 55.

Habari Nyingine: Watangazaji 12 wa kike tajika ambao mapenzi yao yaliporomoka machoni petu

Habari Nyingine: GSU wakabiliana na maafisa wa KDF, nani ndio kusema?

Hii ni baada ya manusura wengine wawili kufariki wakipokea matibabu hospitalini.

TUKO.co.ke inafahamu kuwa miongoni mwa wale waliopoteza maisha yao ni watoto 9, wanawake 15 na wanaume 31.

Kufikia sasa, tayari familia nne zimeweza kutambua miili ya wapendwa wao.

Aidha, hema la dharura kusaidia familia zilizoathirika kutokana na ajali hiyo kuwatambua wapendwa wao limewekwa katika hospitali ya wilaya ya Kericho .

Habari Nyingine: Picha zinazoonyesha Jacque Maribe anajuta kuchumbiwa na Irungu

Basi hilo ambalo limesajiliwa chini ya Western Express Sacco lilisemekana lilikuwa limebeba abiria wengi kupita kiasi na lilikuwa likiendeshwa kwa kasi wakati lilikosa mwelekeo lilipofika kwenye mteremko mkali eneo la Fort Ternan.

Shughuli za uokoaji bado zinaendelea huku kukihofiwa kwamba huenda miili zaidi imekwama kwenye mabaki ya basi hilo.

Habari Nyingine: Mzungu anaswa kwenye video akiwakabili walinzi, alikataa kutia saini kitabu cha wageni

Kulingana na kamanda wa polisi mkoa wa Bonde la Ufa, waliojeruhiwa walikimbizwa hospitalini na wanaendelea kupokea matibabu.

Read: ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke Tazama habari zaidi kutoka TUKO TV

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibYV3fpJmmKOZnJ56o63RmpmaqpGjtm63xKugnKCfYsSiwM6tpmZxXayur63WmqKeZWFqeq%2BtjLCYp5mlorJuf5Bmrpqekae2rLWNoaumpA%3D%3D

 Share!