Hospitali ya Aga Khan yakosolewa kumwacha mgonjwa nje ya lango lao

-Hospitali ya Aga Khan ilikana kumtelekeza Kibibi Abdulla kama ilivyodaiwa na mamake Christine Obaga -Hospitali hiyo ilisema Kibibi aliachiliwa kwenda nyumbai Alhamisi, Oktoba 25, 2012 lakini akakataa kuondoka hospitalini humo

-Hospitali ya Aga Khan ilikana kumtelekeza Kibibi Abdulla kama ilivyodaiwa na mamake Christine Obaga

-Hospitali hiyo ilisema Kibibi aliachiliwa kwenda nyumbai Alhamisi, Oktoba 25, 2012 lakini akakataa kuondoka hospitalini humo

-Mamake Kibibi alishtaki hospitali hiyo baada ya bintiye kupata matatizo baada ya kufanyiwa upasuaji

-Alipoteza kesi hiyo na alihitajika kuchukua bintiye kutoka hospitalini, lakini akakataa

-Hospitali hiyo ilisema bili ya Kibibi ilikuwa imefikia KSh 49 milioni

Habari Nyingine: Pasta akamatwa akifanya maombi na wanawake 7 wakiwa uchi nyumbani kwake

Hospitali ya Aga Khan imekana madai ya mwanamke mmoja anayeishi Kileleshwa kwamba ilimtelekeza bintiye nje ya lango la nyumba yao kwa kusema aliachiliwa kwenda nyumbani miaka sita iliyopita lakini mamake alikataa kumchukua.

Hospitali hiyo ilisema kuwa Kibibi aliachiliwa kwenda nyumbani 2012 lakini akakataa kuondoka baada ya mamake kukataa kumchukua hata baada ya kupigiwa simu mara kadhaa.

Habari Nyingine: Watangazaji 12 wa kike tajika ambao mapenzi yao yaliporomoka machoni petu

Taarifa kutoka hospitalini humo ilionyesha kuwa binti huyo aliye na miaka 40 alikuwa na bili ya KSh 49 milioni na alikuwa akikaa hospitalini humo kinyume na sheria.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Mamake Kibibi, Christine Wendo Obaga awali kwa vyombo vya habari alisema kuwa hospitali hiyo ilimfukuza bintiye baada ya kushindwa kumfanyia upasuaji.

Habari Nyingine: Mama avua nguo nje ya ofisi ya Uhuru kulalamika 8% VAT

“Hakuna barua zinazoonyesha kuwa aliachiliwa kwenda nyumbani kwa njia inayostahili. Alitupwa hapa akiwa bado amevaa nguo za hospitali. Kesi kuhusu kutelekezwa bado imo kortini,” alisema Dkt Obaga Ijumaa Oktoba 5.

Read ENGLISH VERSION

Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke ,kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News

Subscribe to watch new videos

Subscribe to Tuko youtube channel to watch more interesting videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibYVygZRmn6iroJ7BorjIZrCaZZGcrm63x5qlZrGRoLy0u8uerpplm6q6uK3CoZhmpZeku6vDwGalo51drq5uuMCnnqhlnJa8b7TTpqM%3D

 Share!