-Kinara wa NASA Raila Odinga alikula kiapo fupi mbele ya mamia ya wafuasi wake katika bustani ya Uhuru jijini Nairobi
-Aliapa kuwa ‘Rais wa Wananchi’ na kuapa kuitetea katiba ya Kenya
-Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi na Moses Wetangula hawakuhudhuria hafla hiyo, hali iliyoifanya kuonekana kama hafla ya chama cha ODM
Jumanne, Januari 30, kinara wa NASA Raila Odinga alitimiza ahadi yake alipoapishwa katika bustani ya Uhuru, wiki tisa baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuapishwa siku ya Jumanne, Novemba 28, 2017,
Tofauti na maneno ya kiapo ya kawaida, kiapo cha Raila Odinga kilikuwa fupi na chenye maneno 90 kwa lugha ya Kiingereza.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Habari Nyingine: Wafuasi wa NASA wajaza Uhuru Park kushuhudia Raila akiapishwa
Habari Nyingine: Mambo 14 ya uongo ambayo wazazi huwaambia watoto wao
TUKO.co.ke ilipata maneni yaliyotumiwa katika kiapo hicho ambapo Raila aliapa kuilinda na kuitetea katiba ya Kenya.
Hii hapa matini ya kiapo hicho:
“Mimi, Raila Amollo Odinga, kwa kutambua kikamilifu wito kuu nachukuwa nafasi ya Rais wa jamhuri ya Kenya, ninaapa kuwa nitakuwa mwaminifu na kuwatetea watu na jamhuri ya Kenya; kuwa nitaitetea na kuilinda katiba ya Kenya, kama sheria zilizomo na sheria zingine za jamhuri hii inayotumiwa na watu wa Kenya; kwamba nitaitetea na kuilinda uhuru, uadilifu na heshima ya watu wa Kenya.”
Habari Nyingine: Hutoweza 'kutoboa' 2022 bila ya msaada wangu - Raila amwambia Ruto
Raila alikaribishwa kwenye jukwaa na seneta wa Siaya James Orengo na kwa haraka akalishwa kiapo na Miguna Miguna na mbunge wa Rauaraka T.J Kajwang.
Habari Nyingine: Mke wa mhubiri amwanika mumewe kanisani akisema ana wapenzi wengi
Baada ya kuonyesha cheti chake kwa umma, Raila alitoa hotuba yake ya kwanza akiahidi kufichua kwa nini vinara wenzake walikosa kuhudhuria hafla hiyo.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una taarifa ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Je, unaunga mkono kuapishwa kwa Raila Odinga? – Kwenye TUKO TV
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4F3f5JmpJqmlaO8bsXApaCyp6SquqrDwGairqWnlr2qv8eaZKuZmaGub7TTpqM%3D