- Moses Kuria amemkosoa Raila Odinga baada ya kutangaza tarehe ya uapisho wake
-Kuria alisema kuwaRaila amepoteza mwelekeo wa kisiasa na hakuna siku atakuwa rais wa Kenya
-Raila na viongozi wengine wa NASA walifurushwa na maafisa wa polisi kabla ya kumaliza kuwahutubia wafuasi wao katika uga wa Jacaranda
Mbunge wa Gatungu Kusini Moses Kuria amemkosoa vikali Raila Odinga baada ya kutangaza kuwa ataapishwa kama rais wa bunge la wananchi Desemba 12.
Habari Nyingine:Picha 16 za zamani za Uhuru, Raila na wanasiasa wengine; zitakusisimua mno
Kulingana na maoni ya Kuria Raila amepoteza mwelekeo na hakuna siku atakuwa rais wa Kenya.
Raila na wafuasi wake walisusia sherehe ya uapisho wa rais Uhuru Kenyatta na badala yake waliandaa mkutano wa maombi maalum wa kuwakumbuka wafuasi wao waliofariki wakati wa maandamano.
Hata hivyo,mkutano huo hakufanyika kwa utaratibu kwani ulitatiziwa na maafisa wa polisi waliowatawanya wafuasi wake.
Habari Nyingine: Jamii ya wafanyibiashara jijini Nairobi yaanda karamu ya nyama choma baada ya Uhuru kuapishwa
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pinzi zinapochipuka
" Tafadhali muombeeni Raila,amepoteza mwelekeo sana na anapaswa kuona daktari kubaini iwapo yuko na akili timamu, Kuria aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
TUKO.co.ke imeweza kubaini kwamba Raila alifululiza hadi mtaa wa Kibra baada ya kufurushwa Jacaranda na baadaye kuwahutubia wananchi katika mtaa huo.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiaoZygJhmqZqhnJZ6ornEqaatnaqWeq7DxKWcpJ2fYriirsismK2Zlpaxqa3LomSmrZ%2Bir6a6yGakqKuVqHqswdGimGegpKK5